VIDEO : AIDA KENANI AIPONGEZA WIZARA YA MAJI ,ATAKA FEDHA KUKAMILISHA MIRADI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 8, 2025

VIDEO : AIDA KENANI AIPONGEZA WIZARA YA MAJI ,ATAKA FEDHA KUKAMILISHA MIRADI



Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Aida Kenani, ameishauri Serikali kuonesha dhamira ya dhati katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika mkoa wa Rukwa, hususan katika mamlaka ya mji mdogo wa Namanyere, ambako amesema kiwango cha upatikanaji wa maji bado kipo chini ya asilimia 50.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/26, iliyowasilishwa na Waziri Jumaa Aweso, Mbunge Kenani alieleza kuwa pamoja na Serikali kupeleka miradi ya maji katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Nkasi, bado baadhi ya maeneo yanaendelea kukabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa maji.

“Mheshimiwa Waziri, jambo hili nimelizungumza kwa miaka mitano. Suluhisho la msingi ni kutoa maji kutoka Ziwa Tanganyika na kuyasambaza katika mkoa wa Rukwa. Sasa tunataka kujua, hili jambo limefikia wapi?” amesema Kenani.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kupongeza Waziri Aweso, Naibu wake na Katibu Mkuu wa Wizara kwa uadilifu na utendaji wao wa kazi, lakini akasisitiza kuwa mafanikio yoyote hayawezi kufikiwa iwapo wizara haitapatiwa fedha za kutosha.

Kenani ameitaka Serikali kuangalia pia uwezekano wa kutekeleza miradi ya muda mfupi wakati miradi mikubwa ya muda mrefu kama wa Ziwa Tanganyika ikiendelea kufanyiwa utekelezaji.


No comments:

Post a Comment