Lusaka, Zambia
Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt Gen Mathew Edward Mkingule, amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, waliofika Ubalozini leo tarehe 12 Mei, 2025 asubuhi kwa ajili ya kujitambulisha. Wataalamu hao wapo nchini Zambia kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa Hospitali ya Kufundishia ya Zambia (University Teaching Hospital - UTH) kuhusu huduma ya uchujaji wa damu kwa njia tumbo (Peritoneal Dialysis).
Katika mazungumzo yake na ujumbe huo Mhe. Balozi Lt Gen Mathew Edward Mkingule aliwakaribisha wataalamu hao waliobeba bendera ya Tanzania, akisema kuwa ni fursa muhimu kwa nchi yetu kushiriki katika kubadilishana utaalamu wenye lengo la kuboresha huduma za afya Barani Afrika. Pia, ameshukuru na kupongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hasan kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya afya nchini Tanzania.
"Nawashukuru mmekuja hapa Zambia na mmeona wenyewe na mtafanya ulinganifu, tunayo haki ya kupongeza Serikali ya Tanzania kwa maboresho makubwa katika sekta ya afya yenye nia ya kutoa huduma bora na za kibobezi kwa wananchi wetu pamoja na mataifa jirani. Hii imeifanya Tanzania kuwa kimbilio la nchi nyingi za ukanda wa SADC zinazohitaji huduma za kibingwa na bobezi, hususan katika masuala ya uchujaji wa damu na huduma za magonjwa sugu," alisema Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule.
Ameongeza kuwa, "Huduma hizi zimeboreshwa sana, ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo maalum vya huduma za afya kuanzia ngazi ya Vituo vya Afya, Zahanati, Hospitali kwa kuimarisha miundombuni ya kutolea huduma za afya, ununuzi na ufungaji wa vifaa tiba vya kisasa, pamoja na kuwajengea wataalamu uwezo wa ndani na wa kimataifa. Hii inatoa mwanga wa matumaini kwa wananchi wa Tanzania na jirani zao." – Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule.
Kwa upande wake, Kiongozi wa timu hiyo ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , Dkt. Octaben Kasanga, Daktari Bingwa wa Afya na Magonjwa ya figo, amemshukuru Mhe. Balozi Lt Gen Mkingule kwa ushirikiano na mapokezi mazuri waliyopatiwa kutoka kwake na Maafisa wa Ubalozi. Timu hiyo ya wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wameahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za tiba na sekta ya afya kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania.
"Tunashukuru sana Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Wizara ya Afya, Ubalozi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwezesha kushiriki mafunzo haya muhimu katika Hospitali ya Taifa ya Zambia. Lengo letu ni kujifunza zaidi kuhusu teknolojia na mbinu bora za uchujaji wa damu kwa njia tumbo, ili tuweze kuboresha huduma zetu nyumbani Tanzania," amesema Dkt. Kasanga.
Amesema kuwa hii ni hatua nyingine muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya afya, ambapo Tanzania inaendelea kuonesha njia ya kuwaweka wananchi wake na nchi jirani katika mstari wa mbele wa huduma bora za kibingwa.
Ziara hii ya mafunzo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia WIzara ya Afya na Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kuhakikisha inawaendeleza Watumishi wa Seta ya Afya ndani na nje ya nchi ili waweze kutoa huduma za afya zenye viwango vya kimataifa, na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya katika ukanda wa SADC.

No comments:
Post a Comment