
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete ahani msiba wa Hayati Cleopa Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam leo 10 Mei, 2025.
Dkt. Kikwete ameungana na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Gerson Msigwa pamoja na waombolezaji wengine.










No comments:
Post a Comment