Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo,akiwasilisha leo Mei 14,2025 bungeni jijini Dodoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.

Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Viwanda na Biashara imepanga kutekeleza vipaumbele saba katika bajeti ya 2025-2026 ikiwememo kuwezesha uanzishwaji na uendelezaji wa Viwanda nchini.
Vipaumbele hivyo vimetajwa leo bungeni Mei 14,2025 na Waziri wa Wizara hiyo,Selemani Jafo wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Jafo amevitaja vipaumbele vingine ni kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati,kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuboresha mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mitaa ya viwanda (Industrial Clusters) kwa ajili ya viwanda vidogo na vya kati.
Pia, Kuboresha mazingira ya biashara na kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi;Kuendelea na utafutaji wa masoko kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini; Kuchochea Maendeleo ya watu kwa kuboresha miradi na programu kwa Jamii inayohusisha elimu na Mafunzo ya Ujuzi.
Kipaumbele kingine ni Kuimarisha Usimamizi wa Ubora na Usalama wa Bidhaa Nchini zikiwemo bidhaa za chakula na vipodozi.
No comments:
Post a Comment