WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA MFUMO WA UNUNUZI WA UMMA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 9, 2025

WATU WENYE ULEMAVU WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA MFUMO WA UNUNUZI WA UMMA.


Na Edward Winchislaus, Dodoma.



Serikali imesema imeendelea kuweka mifumo bora ya fursa za kiuchumi,kijamii na katika  uongozi kwa watu wenye ulemavu na makundi maalum nchini na kuwataka kuchangamkia fursa hizo kila zinapo tangazwa.


Hayo yameelezwa leo Mei 9,2025 jijini  Dodoma na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu ( Kazi,vijana,Ajira na wenye ulemavu) Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati alipomwakilisha Naibu Waziri mkuu na waziri wa Nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko aliyetarajiwa kuwa mgeni rasm katika  ufunguzi wa kongamano la kitaifa la watu wenye ulemavu.


Mhe.Ridhiwani amesema licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau katika kuhakikisha kundi la watumaalum wanapata haki sawa na watu wengine lakini  baadhi yao wamekuwa na hali ya kutojiamini katika fursa hizo.


"Juhudi za serikali katika kukuza na kuendeleza ustawi wa watu wenye ulemavu tumezindua mpango kazi  wa Taifa wa Haki na ustawi kwa watu wenye ualbino ( mwaka 2024/2025 hadi mwaka 2028/29) ili kuhakikisha jamii ya watu wenye ualbino wanaishi katika mazingira salama na kushiriki katika shughuli za kijamii,kisiasa,kiuchumi kwa utulivu na amani.


"Lakini pamoja na jitihada za serikali na wadau bado zipo changamoto zinazowakanili kundi hili la watu wenye ualbino kama baadhi yao kutokujiamini, hivyo serikali imeweka mifumo mizuri ya fursa za kiuchumi,kijamii na uongozi hivyo watu wenye ulemavu wajitokeze kuchangamkia fursa hizo,"amesema.


Pia amesema katika kuhakikisha watu wenye ulemavu  wanaendelea kupata haki na ustawi wao serikali imekusudia kukamilisha mapitio ya sera ya Taifa ya huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 ili waweze kwendana na hali ya sasa pamoja na kukamilisha muongozo wa kitaifa wa viwango vya ufikivu kwa watu wenye ulemavu.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma Bw.Daniel Simba amesema jumla ya Makundi Maalum 335 yamekamilisha usajili na uhuishaji wa taarifa zao katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma (NeST) ambapo vijana ni vikundi 204 sawa na 61%, Wanawake ni Vikundi 108 sawa na 32%, Watu wenye Ulemavu ni vikundi 5 sawa na 2% na Wazee vikundi 18 sawa na 5%.


Aidha amesema tuzo za Mkataba zilizotolewa kwa watu wenye ulemavu ni 446 zenye Thamani ya Tsh.  Bil 15.2  kati ya hizo Makundi ya Vijana yamepata tuzo za Mkataba 262 zenye thamani ya Bil 8.2 sawa na 54% , Makundi ya Wanawake yamepata tuzo za Mkataba 151 zenye thamani ya Bil 5.6 sawa na 37%, Makundi ya Watu wenye Ulemavu yamepata tuzo za Mkataba 14 zenye thamani ya Mil 174 sawa na 2% na Makundi ya Wazee yamepata tuzo za Mkataba 19 zenye thamani ya Mil 1.1 sawa na 7%.











No comments:

Post a Comment