📌 Ahaidi ushirikiano wa Serikali na wadau.
📌 Aishukuru Kamati ya Kitaifa iliyoongozwa na Bi. Sara Masasi kwa kufanikisha maadhimisho hayo.
📌 Asema historia imeandikwa maadhimisho Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2025
Na WMJJWM-Dar Es Salaam
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amewashukuru wadau wadhamini na Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Mwaka 2025 inayoongozwa na Bi. Sara Masasi kwa kufanikisha maadhimisho hayo.
Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo Mei 12, 2025 wakati wa hafla ya kuwashukuru wadau, wadhamini na Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho hayo iliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
Waziri Dkt. Gwajima amesema Maadhimisho ya mwaka huu yamefanikishwa kupitia udhamini wa wadau, Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi na kuwashukuru wadhamini kwa michango yao ya kifedha na vifaa iliyowezesha maadhimisho hayo kwa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Wanawake nchini.
Amesema Maadhimisho hayo hayakuwa tu sherehe bali yalikuwa jukwaa la kutafakari, kuhamasisha na kusherehekea mafanikio ya wanawake katika kipindi cha miaka 30 ya utekelezaji wa maazimio ya ulingo wa Beijing katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
"Kwa niaba ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara anayoiongoza huku akiwashukuru kwa kuweka
historia na historia hiyo haitasahaulika na amewaomba kuendelea kushirikiana katika safari ya kuwawezesha wanawake kwa vitendo kwa sauti na kwa upendo." amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu amewasihi wadau hao kuendelea kushirikiana katika kupeleka mbele ajenda ya kumwezesha mwanamke na kukuza usawa wa Kijinsia hasa kwa kufanya kazi pamoja katika utekelezaji wa ajenda hizo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake 2025 Bi. Sara Masasi ameishukuru Serikali kupitia Wizara kwa kuwaamini katika maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na amehaidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za maendeleo.
Mmoja wa wadau kutoka Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Adam Mihayo amesema Benki hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono ajenda mbalimbali hasa katika kuwawezesha Wanawake kiuchumi kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa na ne Benki hiyo.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekutana na wadau wadhamini na Kamati ya Maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa Mwaka 2025 kwa lengo la kufanya thathimini ya Maadhimisho hayo na mipango ya kuboresha zaidi kwa miaka ijayo.
No comments:
Post a Comment