WAZIRI LUKUVI AMWAKILISHA RAIS DKT.SAMIA KATIKA SHEREHE ZA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KUU KATOLIKI LA TABORA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, May 25, 2025

WAZIRI LUKUVI AMWAKILISHA RAIS DKT.SAMIA KATIKA SHEREHE ZA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MSAIDIZI WA JIMBO KUU KATOLIKI LA TABORA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi ameungana na waumini wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora katika Ibada ya Misa Takatifu ya kumuweka wakfu Mhashamu Josephat Jackson Bududu kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo.

Sherehe hiyo imefanyika leo, tarehe 25 Mei 2025, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia mjini Tabora, ambapo Mhe. Lukuvi alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment