ZINGATIAENI VIWANGO NA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA – DKT MFAUME. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 3, 2025

ZINGATIAENI VIWANGO NA UBORA WA HUDUMA ZA AFYA – DKT MFAUME.



OR-TAMISEMI


Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amewataka watumishi wa afya katika ngazi ya msingi kuzingatia viwango (SOP) na ubora wa huduma za afya katika utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt. Mfaume amesema hayo alipokuwa akikagua hospitali ya halmashauri ya manispaa ya ubungo katika ziara yake ya kikazi inayoendelea mkoani Dar es Salaam yenye lengo la kuangalia upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii.

“Wakati tunatoa hamasa kwa wananchi wanapokuja katika maeneo yetu kupata huduma lazima na sisi kama watendaji tuwe mfano kwa kuishi viwango vya ubora katika kutoa huduma bora na Salama” amesema Dkt.Mfaume

Amesema kwa kuzingatia viwango vya utoaji huduma katika maeneo ya kutendea kazi itasidia kumlimda mtoa huduma za afya na kumlimda mteja anayepokea huduma.

Aidha, Dkt. Mfaume amesema watumishi wanaofanyakazi kwa kukiuka misingi na viwango vya utoaji wa huduma za afya anafanya kosa kisheria kwani viwango hivyo vimekubalika kitaifa na kimataifa kupitia vyama vya taaluma na bodi taaluma zinazowasimamia watumishi hao.




No comments:

Post a Comment