ANNE MAKINDA ATAKA TAKWIMU ZITUMIKE KURATIBU HUDUMA KWA WAZEE NCHINI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, June 14, 2025

ANNE MAKINDA ATAKA TAKWIMU ZITUMIKE KURATIBU HUDUMA KWA WAZEE NCHINI.



Na WMJJWM- Shinyanga


Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda amesema takwimu ni muhimu katika uratibu na utoajia wa huduma kwa wazee nchini.

Makinda amesema hayo tarehe 14 June 2025, mkoani Shinyanga wakati akiwasilisha mada katika Kongamano la Siku ya Kimataifa Kuelimisha na Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee.

" Ili huduma kwa wazee ziweze kutolewa kwa ufanisi ni muhimu kutumia takwimu zilizopo katika Halmshauri zetu, ili kujua wazee wangapi hawajiwezi kabisa na wangapi wanaojiweza na kuweka utaratibu wa kutoa huduma kwao" amesema Makinda.

Makinda ambaye ni Kamisaa wa Sensa ya Taifa ya mwaka 2022, ameeleza kwamba wazee ni rasimali muhimu, kwasababu wamelitumikia Taifa hivyo ni wajibu kuzingatia ustawi wao ikiwemo huduma za afya na matunzo.

Mmoja wa Mzee anayeishi katika Makao ya Wazee Kolandoto Shinyanga, Ditto Msola akichangia mada katika Kongamano hili amemshukuru Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ili kusimamia maslahi ya wazee nchini.


No comments:

Post a Comment