MATI SUPER BRANDS LTD YATOA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU KWA MADEREVA WA BAJAJI . - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 13, 2025

MATI SUPER BRANDS LTD YATOA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU KWA MADEREVA WA BAJAJI .



Na Ferdinand Shayo ,Manyara


Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited yenye makao Makuu mjini Babati mkoani Manyara imetoa zawadi ya fedha Taslimu kwa madereva wa Bajaji waliobandika matangazo ya kinywaji cha Tanzanite Royal Gin kinachozalishwa na kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kuunga mkono juhudi za vijana wanaojikwamua kiuchumi na kuiunga mkono kampuni hiyo ya wawekezaji wazawa.

Wakikabidhi zawadi kwa madereva wa bajaji ikiwa ni muendelezo wa kutoa zawadi baada ya Mkurugenzi wa Kampuni hiyo David Mulokozi kukabidhi zawadi ya Bajaji mpya kwa kijana aliyeweka picha yake na picha ya bidhaa ya Strong Dry Gin kwenye bajaji yake julai mwaka 2024.

Meneja Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa zawadi kwa madereva wa bajaji ambao ni wabunifu na wamekua wakiweka picha ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo katika bajaji zao kutokana na mapenzi mema waliyonayo kwa kampuni hiyo.

“Tumekua tukipishana na Bajaji zenye picha ya kinywaji cha Tanzanite Royal Gin hapa mjini baada ya kufuatilia kwa kipindi kirefu tumegundua hawa vijana wana damu ya Mati Super Brands Limited hivyo tutaendelea kuwaunga mkono kila mara ,tunatoa wito kwa madereva wengine kuendelea kutuunga mkono” Anaeleza Mpoma.

Meneja Chapa wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited Izack Piganio amesema kuwa wamewakabidhi madereva wa bajaji fedha za mwezi mzima ambazo wamekua wakirejesha kwa wamiliki wa bajaji ili fedha wanazozipata wazitumie kwa maendeleo yao binafsi kama faida kwao .

Piganio amesema kuwa kampuni hiyo inatambua na kuthamini mchango wa madereva wa bajaji katika kutangaza bidhaa bora zinazozalishwa na kampuni hiyo zenye viwango vya kitaifa na kimataifa.











No comments:

Post a Comment