
SERIKALI imeanza hatua ya kimkakati kuhakikisha tunakua na Utalii endelevu kwa kuzingatia mabadiliko yanayoendelea kutoka kuwa nchi ya kipato cha chini hadi nchi ya kipato cha kati cha juu.
Mkakati huu unaenda sambamba na mikakati ya awali na hatua mbalimbali zilizoanza kutekelezwa zinazokusudia kuendeleza sekta ya utalii, kusaidia uhifadhi na maisha ya watu kupitia uhifadhi na utalii.
Akizungumza katika warsha ya kujadili kuhusu Uhifadhi na Mchango wake katika Utalii na Maendeleo ya Jamii Tanzania', Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Tanzania inapotoka katika nchi ya kipato cha chini hadi kipato cha kati mabadiliko makubwa yanatarajiwa na kama nchi hatutikiwi kuendelea kutegemea fedha za misaada na ruzuku pekee bali kuwa mshirika wa kimkakati katika maendeleo.
Dkt. Chana amesema lazima tuhakikishe tunakua na Utalii endelevu utakaomnufaisha kila mmoja wetu , licha ya mafanikio yaliyopatikana kwa upande wa wageni na mapato, juhudi zaidi zinahitajika ili kuweza kuongezeka maradufu kwa idadi na wageni na mapato yetu kwa ujumla na kuhakikisha pia jamii inanufaika.
"Nchi yetu inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya simba, chui, nyati na tunashika nafasi ya 3 duniani kwa kuwa wengi na Tembo, tuna tamaduni na ukarimu wa kuvutia; fukwe bora na viumbe wa baharini; maziwa mengi ambayo yanaweza kutumika kuimarisha utalii na kusaidia sekta nyingine za maendeleo,"
"Ninaamini kuwa warsha hii itakuwa jukwaa muhimu katika kubadilishana mawazo, mitazamo, kubadilishana uzoefu na utaalamu kuhusu uhifadhi na utakaosaidiq kukuza utalii na kuboresha maisha ya watanzania," alisisitiza
Dkt. Chana ameitaka Wizara kuendeleza Tafiti katika sekta ya utalii ambao utaliwezesha Taifa kuwa katika nafasi nzuri ya ya kunufaika na Utalii huku ikiendelea kuhifadhi rasilimali zake.
Tusiridhike na mafanikio tuliyopata kama ongezeko la wageni kutoka milioni 1.7 mwaka 2021 hadi milioni 5.3 mwaka 2024 na mapato ya utalii kuongezeka kutoka bilioni 1.3 hadi Dola za Kimarekani bilioni 3.9 ila tuongeze jitihada tupate mafanikio zaidi ya haya.
Warsha hii imeandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Ushirikiano na Benki ya Dunia nanunafanyika katika jiji la Arusha kuanzia tarehe 13 - 14 Juni, 2025 ukiwa na lengo la kuangazia namna Tanzania inavyoweza kuboresha maendeleo ya sekta ya utalii, kusaidia uhifadhi na kuboresha maisha ya watu wkupitia uhifadhi na utalii.
Warsha hiii ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuendeleza na kutekeleza mikakati ambayo inaimarisha utengenezaji wa mapato ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa.




No comments:
Post a Comment