MAVUNDE ALIOMBA JESHI LA POLISI DODOMA KUWAFANYA MAAFISA USAFIRISHAJI KUWA MARAFIKI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 10, 2025

MAVUNDE ALIOMBA JESHI LA POLISI DODOMA KUWAFANYA MAAFISA USAFIRISHAJI KUWA MARAFIKI



Na Okuly Julius DODOMA


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amemuomba Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi George Katabazi, kuhakikisha Jeshi la Polisi linawafanya Maafisa Usafirishaji kuwa marafiki wa karibu wa Jeshi hilo.

Mhe. Mavunde alitoa wito huo Juni 10, 2025, jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chama cha Ushirika cha Madereva wa Pikipiki Dodoma (UMAPIDO SACCOS).


"Umekuja na programu nzuri sana ya kushirikisha jamii. Natamani Afisa Usafirishaji wa Mkoa wa Dodoma akimuona askari wa Jeshi la Polisi asimkimbie, bali amuone kama rafiki yake. Mwenyekiti wa bodaboda Chacha awe huru kuonana na Afande RPC ili changamoto ziweze kutatuliwa. Huko ndiko kujenga urafiki wa kweli," alisema Mavunde.

Ameongeza: "Kwa nini nasisitiza hili? Sisi tuna ofisi zetu, lakini wao ofisi zao ni pikipiki na bajaji. Njia bora ya kuwasaidia wafanye kazi zao kwa uhuru ni kuwafanya wawe marafiki zetu."

Kuhusu SACCOS hiyo, Mhe. Mavunde aliahidi kuendelea kuisimamia kwa karibu ili kuwasaidia Maafisa Usafirishaji kunufaika na kazi yao. Aliwataka wale ambao bado hawajajiunga na UMAPIDO SACCOS kujiunga na kutokubali kupoteza fursa hiyo muhimu.

Katika mchango wake kwa chama hicho, Mavunde alitoa shilingi milioni 10, na kufanya jumla ya mchango wake kufikia shilingi milioni 15 na kuifanya SOCCOS hiyo kuanza na milioni 20,100,000. Aliahidi pia kuwajengea uzio wa Ofisi yao ili kuifanya kuwa ya kisasa na salama.

Aidha, alitoa shukrani kwa Benki ya Ushirika (COOP Bank) kwa kuipatia SACCOS hiyo cheti na kuahidi kuendelea kushirikiana na benki hiyo ili kuhakikisha chama hicho kinakua na kusaidia wanachama wake.

Kwa upande wake, Mkuu wa
 Kitengo cha biashara wa COOP Bank, Bw. Yahya Kyabo, alisema benki hiyo imetoa fursa ya mikopo kwa chama cha madereva wa bodaboda jijini Dodoma ili kuwawezesha kuinuka kiuchumi kupitia kazi wanayoifanya.

Aliwahimiza madereva wa pikipiki na bajaji kutumia fursa zilizotolewa, ikiwemo fursa kutoka Ghana, ili kujikwamua kiuchumi na kumiliki vyombo vyao vya usafiri.


Benki hiyo pia ilihimiza madereva kufungua akaunti ili waweze kunufaika na huduma kama mkono wa pole, bima ya afya, na bima kubwa na ndogo kwa usalama wao na familia zao.









No comments:

Post a Comment