PROF. NAGU AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA ZIARA YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA PWANI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 2, 2025

PROF. NAGU AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA ZIARA YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA HUDUMA ZA AFYA MKOA WA PWANI



OR-TAMISEMI


Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia Afya, Prof. Tumaini Nagu, ameongoza kikao kazi cha maandalizi ya ziara ya usimamizi shirikishi kuhusu upatikanaji wa huduma za afya, lishe na ustawi wa jamii katika Mkoa wa Pwani.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Rais – TAMISEMI, Magogoni jijini Dar es Salaam, Prof. Nagu amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kufuatilia hali ya utoaji wa huduma za afya pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na watumishi wa vituo vya kutolea huduma.

Kikao hicho kimeandaliwa na Idara ya Usimamizi wa Huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa jamii kupitia usimamizi shirikishi na majadiliano ya moja kwa moja na wadau wa sekta ya afya.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza kesho, ikianzia katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, kisha kuendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, na kuhitimishwa katika Halmashauri ya Mji wa Rufiji.




No comments:

Post a Comment