
Na. Hellen M. Minja Habari – DODOMA RS
Mkoa wa Dodoma unatajwa kufaidika zaidi na Miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo ya Kimkakati, Maendeleo na ile yenye manufaaya ya moja kwa moja kwa wananchi ambayo imetekelezwa katika ngazi ya Kata hivyo, Uongozi wa Mkoa umeandaa ‘Dodoma Samia Day’ ili wananchi wapate fursa ya kusikia na kuyasema yale yaliyofanyika katika Kata zao.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amebainisha hayo wakati wa Mkutano na Waaandishi wa Habari kwenye ukumbi wa ofisi yake Jijini humu kuzungumzia tukio hilo leo June 02, 2025 ambapo tukio hilo linatarajiwa kufanyika June 03.
“Sisi Mkoa wa Dodoma katika kipindi cha awamu ya sita, tumepokea miradi ambayo imegharimu zaidi ya shilingi Trilioni 10 ya fedha za Kitanzania. Miradi hiyo ni ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa nje KM. 112.3 unaogharimu shilingi Bilioni 221, ujenzi wa barabara ya Ntyuka –Mvumi-Kikombo KM 25 kwa shilingi Bilioni 25”.
Aidha, baadhi ya miradi aliyoitaja ni pamoja na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Zuzu kutoka Megawati 48 mwaka 2020/21 hadi megawati 200 kwa gharama ya shilingi Bilioni 53. Ujenzi wa Mradi wa umeme Zuzu wenye uwezo wa kupooza umeme megawati 32 hadi megawati 200 kwa gharama ya shilingi Bilioni 202.
Mbali na hilo, Mkuu wa Mkoa amesema pamoja na miradi hiyo iliyotekelezwa katika ngazi ya Mkoa (miradi mikubwa ya kimkakati) lakini, ipo miradi iliyotekelezwa kwa ngazi ya Halmashauri, ametaja gharama za miradi hiyo kwa ujumla wake kwa kila Halmashauri ambapo katika Halmashauri ya Bahi, Miradi yenye thamani ya Bilioni 23.9 imetekelezwa.
“Chamwino imetekeleza miradi ya shilingi Bilioni 99.8, Chemba Miradi ya Bilioni 24.1, Jiji la Dodoma miradi ya shilingi Bilioni 151.4, Kondoa miradi ya Bilioni 23.2, Kondoa Mji miradi ya Bilioni 12.4, Kongwa miradi ya Bilioni 55.9 na Mpwapwa miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 77.2” Mhe. Senyamule.
Sanjari na hayo, Mhe. Senyamule ameongeza kuwa, kila Kata imejiandaa kusherehekea siku hiyo kwa namna yake kwani zipo ambazo zimeanzisha mashindano ya michezo mbalimbali ambapo tarehe June 03, 2025, itakua fainali, kad
No comments:
Post a Comment