IAA YAENDELEA KUJIPANGA KUSHIRIKI KIKAMILIFU AFCON 2027 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 19, 2026

IAA YAENDELEA KUJIPANGA KUSHIRIKI KIKAMILIFU AFCON 2027

  


Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kinaendelea kuwaandaa wanafunzi na walimu kushiriki kikamilifu katika kutangaza Tanzania, vitutio vyake vya Utalii pamoja na chuo hicho kupitia Mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kampasi ya Dodoma (IAA), Prof. Epaphra Manamba leo tarehe 19 Juni 2026; wakati akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.

“Ukizungumzia Arusha unazungumza Utalii, makao makuu ya IAA ni Arusha na sisi IAA tuna programu ya utalii na ukarimu; kwa hiyo wanafunzi wetu watashiriki kikamilifu kufanyia kazi yale waliyojifunza katika eneo la utalii na ukarimu kuanzia kuwapokea wageni mbalimbali, kutangaza nchi yetu na vivutio vyake na chuo chetu pia,” amesema Prof. Manamba.

 Aidha, Prof. Manamba amesema IAA inatambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya nchi na itahakikisha inaendelea kuandaa wataalam wa fani mbalimbali ambao watakuwa na uwajibikaji jumuishi kwa ajili ya kushiriki kujenga uchumi jumuishi kuendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

Katika hatua nyingine Prof. Manamba amesema dirisha la maombi kwa ngazi ya Cheti (Certificate), Stashahada (Diploma)  na Shahada ya Uzamili (Master’s Degree ) limefunguliwa, hivyo akatoa wito kwa watu wenye sifa na vigezo vya kujiunga na IAA katika kutuma maombi yao ili waweze kupata elimu bora inayojibu mahitaji ya wakati ya soko la ajira.

Naye Bw. Justine Kitaja ambaye ni mhitimu wa IAA Shahada ya kwanza na Shahada ya Uzamili  ameipongeza IAA kwa ubunifu wa kutoa shahada ya uzamili kwa mwaka mmoja kupitia mfumo mseto (masomo ya darasani na kwa njia ya mtandao/Blended and Physical classes); jambo linalosaidia kuokoa muda na kuwawezesha wanafunzi kusoma  huku wakiendelea na majukumu yao ya kazi na familia.







No comments:

Post a Comment