
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amezindua duka la mkaa rafiki eneo la Nzuguni Jijini Dodoma lenye lengo la kuhakikisha kila Mtanzania anapika kwa Nishati safi na kulinda afya na mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo hasa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, lengo ni kuhakikisha takribani asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ifikapo mwaka 2034.
Uzinduzi wa duka hilo umefanyika siku ya Juni 24,2025 kwa kusimamiwa na Shirika la Madini Taifa (STAMICO) pamoja na Shirika lisilo la kiserikali Foundation for Disabilities Hope.

RC Senyamule amesema Kati ya makundi unayoathirika na nishati isiyo safi mojawapo ni kundi la watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo duka hilo litakuwa nisehemu ya utatuzi wa Changamoto yao.
Pia mewahasa watu wenye uhitaji maalum kuendelea kujipambanua kwa kujifunza kwa vijana ambao wamejipambanua kuwasaidia ili kuondoakana na mazingira magumu na tegemezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amesema kwasasa wanao mpango wa kusambaza makontena ya kama hayo nchi nzima kwa taasisi za wanawake na Samia ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi katika maeneo yote nchini.
"Tunayo makontena 23 tayari ambapo Saba tumekwisha kuyasambaza lakini huo ni mwanzo tunakwenda mkoa kwa mkoa kuzindua maduka kama haya ili kila mtu, kila mkoa popote pale alipo aweze kupata nishati safi ya kupikia, "amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya FDH Maiko Salali amesema manufaa ya huo ni kuhakikisha kwamba kundi la watu wenye ulemavu hasa wenye Ualbino ambao wamekuwa wakipata athari kubwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti.
"Sisi tunaenda kufaidika kwanza kujiinua kiuchumi lakini pia tunaenda kuongeza muda mrefu kwa watu wenye ualbino kuishi kwasababu watakuwa wameweza kuondokana na zile athari za mionzi ya jua ambazo zinatokana na ukataji wa miti,"amesema.





No comments:
Post a Comment