SIMBACHAWENE: TAASISI ZA UMMA ZITUMIE MIFUMO YA KIDIJITALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 17, 2025

SIMBACHAWENE: TAASISI ZA UMMA ZITUMIE MIFUMO YA KIDIJITALI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amezitaka taasisi zote za umma kuhakikisha zinatumia mifumo ya kidijitali katika kuwahudumia wananchi ili kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji.

Amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Utumishi wa Umma 2025, yenye kaulimbiu isemayo “Himiza matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji.”

Simbachawene amesema kuwa Serikali imejenga mifumo mingi ya kidijitali, ikiwemo ya kufuatilia utendaji kazi wa watumishi wa umma, ambayo imeondoa ubabaishaji na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Aidha, amewahimiza wananchi kutumia mifumo ya e-malalamiko na e-mrejesho ili kuwasilisha changamoto wanazokutana nazo, ambapo serikali itazifanyia kazi kwa wakati na kuboresha huduma.

“Nazielekeza taasisi zote za umma kutumia mifumo iliyojengwa ili kurahisisha utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa urahisi,” alisema.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Juma Mkomi, alisema maadhimisho hayo yamehusisha wizara 23, mikoa mitano, halmashauri tatu na taasisi 101 za umma.


Alieleza kuwa kupitia maadhimisho hayo wananchi wanapata fursa ya kuhudumiwa moja kwa moja, kufahamu majukumu ya taasisi mbalimbali na kutoa mrejesho kwa ajili ya kuboresha huduma.







No comments:

Post a Comment