
OR-TAMISEMI, Iringa
Timu ya Netiboli ya Mkoa wa Songwe imeendelea kuonyesha uwezo mkubwa kwenye mashindano ya gUMISSETA kwa kuicharaza Morogoro kwa mabao 38–9 katika mchezo wa hatua ya makundi.
Mchezo huo uliopigwa leo Juni 22, 2025 kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa, ulianza saa nne asubuhi ambapo Songwe ilianza kwa kasi na kumaliza kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa mabao 24–4.
Katika kipindi cha pili, Songwe iliendeleza mashambulizi mfululizo na kuibuka na ushindi mnono wa 38–9 dhidi ya Morogoro.
Katika michezo mingine ya hatua ya makundi, wenyeji Iringa waliwaduwaza Dodoma kwa kuwapiga mabao 30–14, huku Tanga ikiitandika Mtwara kwa mabao 31–12.
Mchezo wa kusisimua uliokutanisha Shinyanga na Katavi ulimalizika kwa sare ya 24–24, wakati Singida iliibuka na ushindi wa 27–20 dhidi ya Pwani. Rukwa nayo iliichapa Lindi kwa mabao 20–10, huku Mwanza ikitoa kipigo kikali kwa Njombe kwa ushindi wa mabao 57–2.
Mashindano ya UMISSETA ngazi ya taifa kwa mwaka 2025 yanaendelea mkoani Iringa, yakiwa katika hatua ya makundi kabla ya kufuzu kwa robo fainali




No comments:
Post a Comment