TANROADS KUPANDA MITI 150,000 KATIKA BARABARA NNE ZA MZUNGUKO WA NJE ZA JIJI LA DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 13, 2025

TANROADS KUPANDA MITI 150,000 KATIKA BARABARA NNE ZA MZUNGUKO WA NJE ZA JIJI LA DODOMA


Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imedhamiria kupunguza gesiukaa kwa kupanda miti 150,000 katika barabara nne za mzunguko wa nje za jiji la Dodoma.

Mratibu wa zoezi la upandaji miti hiyo, Bw. Julius Luhuro amesema tayari imeshapandwa miti 35,000 ya matunda, kivuli na michikichi, inayosimamiwa na askari wa Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Makutupora.

Bw. Luhuro amesema ili kukabiliana na ukame wa jiji la Dodoma tayari visima 11 vimechimbwa na vitaunganishwa katika mfumo wa umwagiliaji wa miti hiyo ili iweze kukua vyema.

Halikadhalika, amesema changamoto.kubwa wanayokumbana nayo katika ukuaji wa miti hiyo, ni wakazi wa maeneo hayo kupitisha makundi makubwa ya mifugo ambayo hula na kukanyaga miti hiyo, ambayo imekuwa ikirudiwa kupandwa mara kwa mara.

Hatahivyo, Bw. Luhuro amesema TANROADS kwa kushirikiana na taasisi nyingine wapo mbioni kuandaa miongozo mbalimbali ya ujenzi, upandaji na utunzaji wa miti zitakazotumiwa Tanzania nzima, sheria ndogo ndogo kwa jiji la Dodoma.

Pia amesema TANROADS kwa kushirikiana na taasisi nyingine ambazo zipo katika mradi wa Kijanisha Dodoma, watatengeneza bustani mbili za kupumzikia wananchi maeneo ya Swaswa na Chimwaga jiji Dodoma






No comments:

Post a Comment