Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetunukiwa Tuzo ya Uhifadhi wa Mazingira kwa mwaka 2025
Tuzo hiyo imetolewa jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani.
Tuzo hiyo inalenga kutambua mchango wa TPDC katika usambazaji wa gesi asilia ya kupikia na matumizi ya gesi asilia kwa njia salama na rafiki kwa mazingira.
Hii ni sehemu ya juhudi za shirika hilo katika kukuza nishati safi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo huchangia uharibifu wa mazingira.
Pia TPDC ilitambuliwa kwa kuendeleza matumizi ya gesi asilia kama mbadala wa nishati chafu, hatua inayosaidia kupunguza hewa ukaa na kulinda afya ya jamii.
No comments:
Post a Comment