TPDC YATUNUKIWA TUZO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, June 8, 2025

TPDC YATUNUKIWA TUZO YA UHIFADHI WA MAZINGIRA 2025

 

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetunukiwa Tuzo ya Uhifadhi wa Mazingira kwa mwaka 2025


Tuzo hiyo  imetolewa jijini Dodoma na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani.


Tuzo hiyo inalenga   kutambua mchango wa TPDC katika usambazaji wa gesi asilia ya kupikia na matumizi ya gesi asilia kwa njia salama na rafiki kwa mazingira.  


Hii ni sehemu ya juhudi za shirika hilo katika kukuza nishati safi na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ambayo huchangia uharibifu wa mazingira.  


 Pia TPDC ilitambuliwa kwa kuendeleza matumizi ya gesi asilia kama mbadala wa nishati chafu, hatua inayosaidia kupunguza hewa ukaa na kulinda afya ya jamii.

No comments:

Post a Comment