ULEGA NA SENYAMULE WAKAGUA MAANDALIZI YA ZIARA YA RAIS MKOANI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, June 13, 2025

ULEGA NA SENYAMULE WAKAGUA MAANDALIZI YA ZIARA YA RAIS MKOANI DODOMA



Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule Juni 13, 2025 wamekagua maandalizi ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itayofanyika Mkoani humo kesho tarehe 14 Juni, 2025.

Mheshimiwa Rais Dkt. Samia atakagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa jiji la Dodoma (km 112.3) pamoja na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato ambapo ataambatana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina.

Akiwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, Waziri Ulega Mkuu na Mkuu Mkoa Senyamule wameshuhudia majaribio ya ndege Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina Bombardeir Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika Kiwanja hicho kuashiria kukamilika kwa barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kiwanja hicho.







No comments:

Post a Comment