
Na. Mwandishi Ubalozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe.
Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Zimbabwe CP Suzan Kaganda amempokea Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), alieongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kikanda wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Ramsar kuhusu usimamizi wa Maeneo ya Ardhi Oevu unaofanyika Victoria Falls, nchini Zimbabwe.
Katika hotuba yake ya ufunguzi Mheshimiwa Rais Dkt. Mnangagwa,amesema kuwa maeneo oevu ni muhimu kuendelezwa na kulindwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Aidha Mheshimiwa Mnangagwa ametoa wito kwa nchi wanachama wa Mkataba wa Ramsar kuhakikisha kuwa, masuala yote yatakayoafikiwa kwenye Mkutano huo yanatekelezwa ili kuhakikisha uhifadhi wa Maeneo ya Ardhi Oevu (Wetlands) yanalindwa vyema.
Nae Mheshimiwa Waziri Mhandisi Masauni ameshiriki Mkutano huo akimuwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo aliambatana na Mhandisi Cyprian Luhemeja, Katibu Mkuu-Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Balozi CP Suzan Kaganda, Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, ambapo alieleza kuwa msimamo wa Tanzania katika kulinda maeneo ya ardhi Oevu utazingatiwa kwa ufanisi mkubwa.
Sambamba na hilo amebainisha kuwa pamoja na kueleza mafanikio na mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuhifadhi maeneo hayo wataendelea kuweka mikakati mizuri katika kuyahifadhi huku washiriki wengine katika mkutano huo ni Dkt. Deogratius Paul, Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Hifadhi ya bioanuai pamoja na wataalam kutoka TAWA, TFS na Tanzania Land Commission.
Mkutano huo umebeba kauli mbiu isemayo “Protecting Wetlands for Common Future”.



No comments:
Post a Comment