CRDB YAPIGA TAFU MAONYESHO YA NANE NANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, July 31, 2025

CRDB YAPIGA TAFU MAONYESHO YA NANE NANE



Benki ya CRDB imekabidhi shilingi Milioni 50 kwa Wizara ya Kilimo ikiwa ni udhamini wake kwa maonesho hayo yanayotarajiwa kuzinduliwa Agosti Mosi Mwaka2025 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza wakati akipokea mfano wa hundi Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli ameishukuru Benki ya CRDB kwa udhamini huo ambao ni chachu katika kukuza Aekta ya Kilimo.

Aidha,Mweli ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Wananchi kwenye banda la Benki hiyo ambalo litakuwa likitoa huduma ya mikopo ya papo kwa hapo wakati wa maonesho hayo.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Kanda ya Kati, Chabu Mishwaro amesema benki hiyo imejipanga kikamilifu katika Maonesho hayo katika kuwahudumia wananchi.


Sanjari na hayo Mishwaro amebainisha kuwa katika kudhihirisha hilo,Benki ya CRDB imeshatoa jumla ya Shilingi Trilioni 1.4 kwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment