Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kuwa jumla ya wapigakura 37,655,559 wamejiandikisha kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.55 kutoka wapigakura milioni 29.7 waliokuwa wamejiandikisha mwaka 2020.
Mwenyekiti wa INEC, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Jacob Mwambegele, ametoa taarifa hiyo Julai 26, 2025, jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kalenda ya Uchaguzi Mkuu, akibainisha kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yanaendelea vizuri na kwa kuzingatia misingi ya uwazi, haki na sheria za nchi.
Katika ratiba hiyo mpya, kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuanza rasmi Agosti 28, 2025, na uchaguzi utafanyika Oktoba 29, 2025.

Ratiba Muhimu ya Uchaguzi: Utoaji wa Fomu za Uteuzi kwa Wagombea wa Urais na Makamu wa Rais:Agosti 9 hadi Agosti 27, 2025, Siku ya Uteuzi wa Wagombea (Rais, Makamu wa Rais, Ubunge na Udiwani):Agosti 27, 2025, Kipindi cha Kampeni Tanzania Bara:Agosti 28 – Oktoba 28, 2025, Kipindi cha Kampeni Zanzibar:
Agosti 28 – Oktoba 27, 2025
(Kupisha upigaji kura wa mapema), Siku ya Kupiga Kura Kitaifa:
Jumatano, Oktoba 29, 2025, amesema Jaji Mstaafu Mwambegele
Aidha, Jaji Mstaafu Mwambegele ameeleza kuwa kutakuwa na vituo vya kupigia kura 99,911 nchini kote, kati ya hivyo vituo 97,349 vitakuwa Tanzania Bara na 2,562 visiwani Zanzibar, ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.49 kutoka vituo 81,467 vilivyotumika mwaka 2020.

Katika hatua nyingine ya kuhakikisha uadilifu wa uchaguzi, Mkurugenzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) , Ramadhani Kailima, amekabidhi orodha ya watu 8,703 waliojiandikisha zaidi ya mara moja katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Jeshi la Polisi, kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Wawakilishi kutoka vyama kumi na nane walihudhuria hafla hiyo na kueleza utayari wao kushiriki uchaguzi kwa amani na kwa mujibu wa sheria. Wamepongeza hatua ya INEC kuweka wazi kalenda ya uchaguzi mapema, wakisisitiza umuhimu wa elimu ya mpiga kura kuendelea kutolewa.

No comments:
Post a Comment