KATAMBI AVUTA FOMU KUTETEA UBUNGE SHINYANGA MJINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 2, 2025

KATAMBI AVUTA FOMU KUTETEA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Mhe. Patrobas Katambi akitoa neno la shukrani baada ya kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mhe. Patrobas Katambi akitoa neno la shukrani baada ya kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mhe. Patrobas Katambi akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini leo Julai 2,2025 wakati kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, amekuchua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania tena nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

Hatua hiyo ni sehemu ya mchakato wa ndani ya chama kwa ajili ya kumpata mgombea atakayepeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akizungumza baada ya kurejesha fomu hiyo leo Julai 2,2025 katika ofisi za CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhe. Katambi ambaye ni Mbunge anayemaliza muda wake, anayewania kutetea nafasi hiyo kwa kipindi kingine, ameeleza dhamira yake ya kuendelea kuwatumikia wananchi wa Shinyanga Mjini kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kushirikiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kunisaidia kufika siku ya leo ikiwa ni hitimisho la miaka mitano ya utumishi katika nafasi ya ubunge. Aidha, namshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, pamoja na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla katika ngazi zote za uongozi kwa kuniamini na kunipa ridhaa ya kuwa kiongozi katika chama hiki pendwa",amesema Mhe. Katambi.

"Nawashukuru sana viongozi wa chama ngazi ya mkoa na wilaya lakini zaidi wana-CCM wote pamoja na wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa kuniamini, kunishauri na kuniongoza, lakini pia kwa kuniambia pasina kificho nini nilipaswa kukifanya kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Shinyanga Mjini",ameeleza.

Mhe. Katambi amesema ana ushahidi na uhakika, na anajivunia heshima kubwa aliyopewa na wananchi wa Shinyanga.

Amesema uaminifu kutoka kwa wananchi, taasisi za dini, bodaboda, mama lishe na makundi mbalimbali, umekuwa chachu kubwa ya mafanikio aliyoyapata katika kipindi chake cha ubunge.

"Hakika nawaambia, katika kipindi cha miaka mitano tumefanikiwa kufanya mambo makubwa, mazito na mengi na kubadilisha sura ya Shinyanga na kuwa jinsi mnavyoiona leo".

"Leo ni shukrani zangu, kama nilivyokuja tarehe 17 ya mwezi wa tano kutoa shukrani kwa wanachama wote wa CCM na viongozi wa CCM, na niliwaambia nawapa shukrani pamoja na kutoa zawadi, nikafanya hivyo. Lakini mkumbuke, kushukuru ni kuomba tena",amesema Mhe. Katambi.

Ameeleza kuwa amerejesha fomu kuomba ridhaa ya kugombea kwa awamu nyingine, akisisitiza kuwa bado ana nguvu na ari ya kuendelea kutumikia chama, serikali na wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini.

"Leo ninatoa neno langu la shukrani kuhitimisha utumishi wangu wa miaka mitano kama Mbunge wa Shinyanga Mjini. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, lakini pia Mhe. Rais Dkt. Samia na Mwenyekiti wa CCM, Katibu Mkuu, Makamu Mwenyekiti wa CCM, mamlaka zote, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, vikao vyote vya CCM, wanachama, viongozi wote wa CCM na wananchi , nawashukuru, wamenipa msaada mkubwa kufanikisha kufanya yote tuliyofanya",amesema Mhe. Katambi

"Na naendelea kuomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika Jimbo hilo, niko tayari kuendelea kuwatumikia, kutumikia chama changu, serikali yangu, lakini pia wananchi wa Jimbo la Shinyanga Mjini",ameongeza Mhe. Katambi.

Aidha Mhe. Katambi amewashukuru waandishi wa habari kwa mchango wao katika kusambaza taarifa na kuwakumbusha pale ambapo kulikuwa na mapungufu ili hatua zichukuliwe.

"Asanteni sana. Pia waandishi wa habari, nanyi pia mmekuwa sehemu ya chachu na changamoto kubwa ya kusaidia kukumbusha pale ambapo hatujafanya, ili twende tukafanye zaidi",amesema.


No comments:

Post a Comment