WAZIRI LUKUVI AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI KWA KUWA WA KWANZA KUHAMIA MJI WA SERIKALI MTUMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, July 23, 2025

WAZIRI LUKUVI AIPONGEZA WIZARA YA MALIASILI KWA KUWA WA KWANZA KUHAMIA MJI WA SERIKALI MTUMBA



Na Okuly Julius, OKULY BLOG, DODOMA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. William Lukuvi, ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwa wizara ya kwanza kuhamia rasmi katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika jengo jipya la wizara hiyo, Mhe. Lukuvi amesema wizara zote zimepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi mpya, lakini baadhi bado wanajikongoja katika utekelezaji.

Aidha, ameupongeza uongozi wa wizara hiyo kwa kuamua kutumia samani zinazozalishwa ndani ya nchi, akibainisha kuwa hilo linaendana na azma ya serikali ya kuhimiza matumizi ya bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wa taifa.

“Ni jambo la kuigwa. Nawapongeza kwa kutumia samani za ndani, kwani ndicho tunachotakiwa kukifanya – kuthamini na kuendeleza bidhaa zetu wenyewe,” amesema Mhe. Lukuvi.

Ametoa wito kwa watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanatunza jengo hilo ili lidumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. 


Vilevile, ameitaka wizara hiyo kuwa mfano kwa wizara nyingine kwa kuhamasisha matumizi ya bidhaa za ndani.




Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, aDkt. Hassan Abbas, amesema ujenzi wa jengo hilo umekamilika kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 20, huku samani zikinunuliwa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 1.6.







No comments:

Post a Comment