DKT. KIMAMBO AWATAKA WATAALAM WA AFYA MUHIMBILI KUFUATA MIONGOZO YA KITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA DAMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, August 18, 2025

DKT. KIMAMBO AWATAKA WATAALAM WA AFYA MUHIMBILI KUFUATA MIONGOZO YA KITAIFA NA KIMATAIFA KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA DAMU


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Dkt. Delilah Kimambo amewataka wataalam wa afya kuendelea kufuatilia miongozo ya kitaifa na kimataifa katika utoaji wa huduma za damu ili kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza kwa wagonjwa wanaofika Hospitalini hapo.

Akizungumza hii leo Jijini Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa mafunzo yanayolenga kujadili na kuelewa madhara yanayoweza kujitokeza kwa wagonjwa wanaoongezewa damu, amesema ni wajibu wa Madaktari, Wauguzi na Wataalam wa Maabara kuijua miongozo ya kitaifa na kimataifa ili kupunguza madhara kwa wagonjwa wanaofika kupatiwa matibabu.

“Ni lazima tuendelee kufuatilia miongozo ya Kitaifa na kimataifa katika utoaji wa huduma za damu, kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa hatari zinazoweza kujitokeza kwa wagonjwa wetu na kuleta sifa mbaya kwetu”, amesema Dkt. Kimambo.

Aidha Dkt. Kimambo amesema matibabu ya damu ni huduma muhimu katika tiba ya magonjwa mbalimbali ikiwemo “magonjwa ya ndani, upasuaji, uzazi salama na saratani”, licha ya mchango mkubwa wa huduma hii katika kuokoa maisha lakini yapo madhara yanayoweza kumpata mgonjwa wakati au baada ya kuongezewa damu.

Hospitali ya Taifa Muhimbili hupokea maombi ya mifuko 120 hadi 150 ya damu kila siku.

No comments:

Post a Comment