Manyara, 31 Agosti 2025 – Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Abdallah Mvungi, amefanya ukaguzi wa maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kikao kazi (retret) cha viongozi wa Wizara hiyo.
Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 1 hadi 4 Septemba 2025 katika Hifadhi ya Ziwa Manyara na Hifadhi ya Ngorongoro.
Maandalizi hayo sasa yamekamilika, tunawakaribisha viongozi wote wa Wizara kushiriki katika kikao hiki muhimu ambacho kitalenga kujadili mipango na mikakati ya maendeleo ya sekta ya maliasili na utalii nchini, sambamba na kutumia muda huo kupumzisha akili na kujenga mshikamano miongoni mwao’ Alisema Bw. Mvungi
No comments:
Post a Comment