RC SENYAMULE AIPONGEZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA NANENANE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, August 5, 2025

RC SENYAMULE AIPONGEZA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA KUTOA MSAADA WA KISHERIA NANENANE



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule ametembelea Banda la Wizara ya Katiba na Sheria katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Jijini Dodoma. Maonesho haya yatafikia kilele chake tarehe 8 Agosti 2025, katika Sikukuu ya Wakulima.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Senyamule ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa juhudi zake za kutoa elimu ya kisheria pamoja na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Ameeleza kuwa huduma hizo ni muhimu katika kuwajengea wananchi uelewa wa haki zao na kuimarisha utawala wa sheria nchini.

Wizara ya Katiba na Sheria inashiriki maonesho haya kwa kutoa elimu kuhusu haki za binadamu, uraia, na utawala bora, sambamba na kutoa msaada wa kisheria bure kwa wananchi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Huduma hizi zimekuwa zikiwafikia wananchi moja kwa moja na kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kisheria wanazokabiliana nazo katika maisha ya kila siku.






No comments:

Post a Comment