Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Rais ya Kimataifa ya Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025 (Presidential Global Water Changemakers Award 2025), heshima kubwa inayotolewa na taasisi ya maji duniani, ( Global Water Partnership) kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika.
Tuzo hiyo imetolewa rasmi na Rais Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tuzo za Rais za Kimataifa za Wabunifu wa Mabadiliko katika Sekta ya Maji 2025, ambapo kwa niaba ya Rais Dkr. Samia, tuzo ilipokelewa na Balozi James Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Tuzo imetolewa wakati wa Mkutano wa Kilele wa Uwekezaji katika Sekta ya Maji wa AU-AIP 2025, ulioanza jijini Cape Town, Afrika Kusini, na unatarajiwa kumalizika tarehe 15 Agosti 2025.
Global Water Partnership imetambua uongozi bora na jitihada za mageuzi za Rais Samia katika sekta ya maji, ikiwemo uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya maji, upanuzi wa huduma ya maji safi kote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na mikakati bunifu ya ufadhili kama vile hati fungani ya Kijani (Green Bond) lililotolewa na Mamlaka ya Maji ya Tanga chini ya Wizara ya Maji
No comments:
Post a Comment