WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA MKOA MWANZA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 15, 2025

WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFUNGA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA MKOA MWANZA



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 15 Agosti 2025, amehitimisha kwa kufunga Mafunzo ya Jeshi la Akiba Mkoa Mwanza, shughuli iliyofanyika katika viwanja vya Mwanankanda wilayani Magu.

Akitoa hotuba yake wakati wa Ufungaji Mafunzo hayo, Dkt. Tax amewataka wahitimu hao kutumia vizuri maarifa na weledi walioupata katika mafunzo hayo ili kukidhi matarajio ya Taifa na malengo ya misingi ya majukumu ya Jeshi la Akiba.

Aidha, amewataka kudumisha nidhamu, Uzalendo na Uhodari katika utekelezaji wa majukumu yao huku wakifahamu kwamba Jeshi la Akiba ni sehemu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Akatamatisha kwa kuwakumbusha Wahitimu na Watanzania kushiriki Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2025, ili kuchagua Viongozi wanaoona watawafaa kuwaletea Maendeleo.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Magu, Mhe Jubilate Lawuo, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, amemshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT kwa kukubali kuwa Mgeni rasmi katika ufungaji wa Mafunzo hayo na amemhakikishia kuwa Uongozi wa Mkoa pamoja na Wilaya ya Magu itawapa kipaumbele Wahitimu hao katika majukumu mbalimbali ndani ya Mkoa na Wilaya za Mwanza pamoja na fursa kwa kadri zitakavyojitokeza.

Naye Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Akiba, Meja Jenerali Erick Mlelwa, amesema Kamandi yake itaendelea kuhakikisha Mafunzo ya Jeshi la Akiba yanafanyika kwa wakati ili kuwaandaa na kuwafunza Askari kwa ajili ya Majukumu ya msingi ya Kijeshi na kusaidia mamlaka za kiraia.


Ufungaji huo wa Mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa Mkoa wa Mwanza yamehudhuriwa pia na Viongozi wa Serikali na Chama kutoka Wilaya Magu na Mkoa Mwanza.





No comments:

Post a Comment