Dkt. Abbasi akagua ujenzi wa Makumbusho ya Jiolojia (Geopark) Karatu - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 18, 2025

Dkt. Abbasi akagua ujenzi wa Makumbusho ya Jiolojia (Geopark) Karatu


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Septemba 18, 2025 ametembelea na kukagua ujenzi wa Makumbusho ya Jiolojia (Geopark) mjini Karatu.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa jengo hilo Dkt. Abbasi ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuboresha baadhi ya historia zilizohifadhiwa katika jengo hilo ili zisomeke kwa usahihi zaidi.

Makumbusho hayo yamekamilika kwa asilimia 100 na yatasaidia watalii kutoka mataifa mbalimbali kufurahia zao la utalii wa miamba kutokana na vivutio vilivyoko katika makumbusho hayo ambapo wakazi wa wilaya za Karatu, Ngorongoro, Monduli na Longido watakuwa sehemu ya wanufaika wa mradi huo.

Jengo hilo lenye thamani ya Tsh. Bilioni 25 litazinduliwa Oktoba mwaka huu.








No comments:

Post a Comment