MAAFISA ELIMU WATU WAZIMA WATAKIWA KUIMARISHA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 16, 2025

MAAFISA ELIMU WATU WAZIMA WATAKIWA KUIMARISHA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI


Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Albert Msovela, amefungua rasmi Kikao Kazi cha Maafisa Elimu ya Watu Wazima wanaotekeleza programu za Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi nchini, ili kuwajengea uwezo katika usimamizi, utekelezaji na utawala bora unaolenga matokeo chanya kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

Bw. Msovela ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, pamoja na wadau wa elimu kwa kuwa na mkutano huo muhimu unaolenga kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu na kwa kuuchagua Mkoa wa Katavi kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima 2025.

Amesema kuwa hatua hiyo ni heshima kubwa kwa mkoa huo, na imetoa hamasa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisomo na kujifunza mbinu mpya zitakazowawezesha kuboresha maisha yao.


Naye, Mratibu wa ELimu ya Watu wa Wazima kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Bi. Felister Mapunda, amesema Wizara inajivunia ushirikiano chanya na wadau katika kutekeleza kwa vitendo Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, Toleo la 2023, huku akisisitiza mshikamano wa kitaifa katika kuadhimisha Siku ya Kisomo Kimataifa na Juma la Elimu ya Watu Wazima kwa maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment