
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2025 amemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika katika ukumbi wa hotel ya Malaika Beach jijini Mwanza.
Washiriki wa kongamano hilo ni wadau wa maendeleo, wakurugenzi wa halmashauri, wataalam kutoka nje na ndani ya Serikali pamoja na viongozi kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika na nje ya Afrika.
kaulimbiu ya Kongamano ni “Kuimarisha uwezo wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa Jamii ili kuwezesha utendaji bora na maendeleo endelevu”.




No comments:
Post a Comment