WANANCHI KYERWA WAFUNGUKA UJENZI WA BARABARA KATA YA MABIRA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 11, 2025

WANANCHI KYERWA WAFUNGUKA UJENZI WA BARABARA KATA YA MABIRA



Na Mwandishi Wetu, Kyerwa


Wananchi wa Kata ya Mabira Wilayani Kyerwa wameipongeza Serikali kwa kuanza ujenzi wa Barabara ya Nkwenda-Mabira kwa kiwango cha lami ambapo wamedai kuwa mradi wa Barabara hiyo ukikamilika wataongezea wateja wa kununua mazao yao na kurahisisha usafiri na usafirishaji.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 umeweka jiwe la Msingi katika Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.0 katika barabara hiyo ambayo inatarajia kukamilika Septemba mwaka huu.

Bw. Ramadhan Robert na Bw. Bosco Gabriel wakazi wa Mabira wamesema wamekuwa wakikutana na athari za vumbi na mali zao kuchafuka hali inayopekelekea kukosa soko hasa mazao kwani yakijaa vumbi ila baada ya ujio wa mradi huo kama wafanyabiashara wamejawa furaha na kudai kuwa mradi huo ukikamilika uende sambamba na taa za barabarani kwa sababu mji huo umeanza kukukua kwa kasi.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kyerwa Mhandisi Yezron Mbasha amesema kuwa mradi huo umegharimu kiasi Cha shilingi Milioni 471.3 ikiwa ni fedha ya serikali inayotokana na tozo za mafuta.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza hadhi ya mji wa Mabira na kusaidia usafirishaji wa mazao kutoka katika eneo hilo hadi maeneo mengine ya wilaya na Kyerwa na wilaya jirani.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza na kulinda Miradi hiyo huku akiipongeza TARURA kwa kutekeleza miradi yenye viwango na yenye ubora ikiwa ni pamoja kuongeza kasi ya upatikanaji wa barabara za lami katika vijiji na maeneo yanayokua kwa kasi.


No comments:

Post a Comment