UFUATILIAJI NA TATHMINI NI NYENZO YA MAENDELEO-MAJALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, September 11, 2025

UFUATILIAJI NA TATHMINI NI NYENZO YA MAENDELEO-MAJALIWA



WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa shughuli za ufuatiliaji na tathmini ni nyenzo muhimu ya kuliwezesha Taifa kufanikisha na kufikia malengo mbalimbali ya kimaendeleo.

Amesema kuwa ni ukweli usiopingika wadau wote na jamii kwa ujumla wakiwa na uelewa wa pamoja kuhusu shughuli za ufuatiliaji na tathmini matokeo ya haraka yatapatikana.

Amesema hayo leo Alhamisi (Septemba 11, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la Nne la Kitaifa la Ufuatiliaji, Tathmini na Kujifunza linalofanyika katika ukumbi wa hotel ya Malaika Beach jijini Mwanza.

Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni kutekeleza kwa vitendo maono ya Rais Dkt. Samia ya kuimarisha upimaji wa utendaji wa Taasisi za Umma, uwajibikaji na kuongeza kasi na uwazi katika kutoa huduma na ustawi wa wananchi kwa ujumla.

“Shughuli za ufuatiliaji na tathmini zinahusisha ukusanyaji, uchambuzi na upimaji wa taarifa kuhusu shughuli zilizopangwa, utekelezaji na matokeo yaliyopatikana. Serikali imekuwa na utaratibu wa kufanya shughuli hii katika vipindi mbalimbali”.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Idara zote zenye dhamana zihakikishe zinakamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa upande wa Serikali zote mbili ili kuwezesha kutungwa kwa Sheria inayokwenda kuongoza Ufuatiliaji na Tathmini

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mamlaka ya Serikali Mtandao kukamilisha Maandalizi ya Mfumo Jumuishi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa kielektroniki. Utakuwa Mfumo Mkuu wa Mifumo yote ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji ndani ya Serikali lengo ni kuweza kuzifuatilia idara za Serikali vizuri, na utawezesha viongozi, watoa maamuzi na wananchi kupata taarifa na takwimu sahihi na kwa muda.

“Watendaji wakuu wote tumieni taarifa zinazozalishwa kutokana na kazi za ufuatiliaji na tathmini ili mfanye maamuzi na kuweka mikakati imara ya kuhabarisha umma juu ya matokeo ya utekelezaji wa kazi za Serikali kwa uhakika zaidi”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa rai kwa Chama cha Wataalamu wa Tathmini Afrika (AfrEA), kuendelea kuzilea TanEA (Tanzania) na ZaMEA (Zanzibar) kwa kuzipa uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwaongoza katika mabadiliko ya kiteknolojia ya utunzaji takwimu na ufuatiliaji.

“TanEA na ZaMEA, endeleeni kujiimarisha na kuongeza kasi ya kuwaunganisha wadau wote muhimu kwa lengo la kubadilishana mawazona uzoefu au kujadili mbinu mpya na bora za zitakazowawezesha kuwafikisha kufanikiwa katika kufanya ufuatiliaji na tathmini wake”.

kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi amesema kuwa katika jitihada zakuimarisha Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini nchini,Ofisi ya Waziri Mku kwa kushirikiana na Mamlaka Mtandao – eGA imefanikiwa kuanza ujenzi wa mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki waufuatiliaji na tathmini “Government Wide Electronic Monitoring and Evaluation System”ambao utapokea taarifa kutoka mifumo mingine na kuzichakata na kuwezesha maandalizi yataarifa ya utendaji wa Serikali.

“Uwepo wa Mfumo huo utawezesha kupokea data, kuzichakata, kuzitafsiri kwa wakati na kuiwezesha Serikali katika ngazi zote kutumia takwimu sahihi katikakupanga, kuboresha afua zinazotekelezwa nakuamua kwa usahihi”.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonaz amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu iliweka msingi imara wa kuimarisha shughuli za ufuatiliaji na tathmini kwa kuanzisha Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali

Amesema kiwa Idara hiyo imeendelea kuwa idara nguzo na muhimu katika kuchangia na kuendeleza juhudi za kuboresha utaalamu wa kufanyia tathmini nchini ambayo imewezesha mashirika ya umma na taasisi mbalimbali kujifunza kutoka katika idara yetu hiyo. “Na tunaamimi kwamba si tu ndani ya nchi bali imeendelea kuwa mwanga hata nje ya nchi, hii ndio nia yetu ya kuifanya iwe kituo cha kujifunza na maarifa”

Kwa Upande wake Muwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Suzan Ngongi amesema kuwa uwazi na uwajibikaji umeiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta za elimu, afya, miundombinu pamoja na mipango ya kupambana na umasikini “Jitihada hizi zimeifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa katika nchi za Afrika Mashariki na Kati”


No comments:

Post a Comment