Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), chini ya uongozi wa Rais Dkt. Patrice Motsepe, limetangaza kurejea kwenye faida baada ya miaka kadhaa ya hasara, likionesha ukuaji mkubwa kutokana na mkakati wa mageuzi ulioanzishwa mwaka 2021.
Tangazo hilo lilitolewa katika Mkutano Mkuu wa 47 wa Kawaida wa CAF uliofanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku ya Jumatatu, tarehe 6 Oktoba 2025.
CAF imeripoti faida halisi ya Dola za Kimarekani milioni 9.48 kwa mwaka wa kifedha wa 2023–2024, ikiwa ni faida ya kwanza kutangazwa baada ya miaka kadhaa. Mafanikio haya yanatokana na ongezeko kubwa la mapato ya kibiashara, mvuto unaoongezeka wa soka la Afrika duniani, kuongezeka kwa wadhamini wapya, pamoja na udhibiti madhubuti wa fedha uliowekwa na uongozi wa CAF.
No comments:
Post a Comment