MAVUNDE AHAMASISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA KIJAMII KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29 MWAKA 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, October 19, 2025

MAVUNDE AHAMASISHA MAKUNDI MBALIMBALI YA KIJAMII KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29 MWAKA 2025


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde ameendelea na mfufulizo wa mikutano ya uhamasishaji wa makundi mbalimbali ya kijamii kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 ambapo leo amekutana na kundi kubwa la 𝙒𝘼𝙈𝙃𝘼𝙉𝙂𝘼 𝙁𝘼𝙈𝙄𝙇𝙔 ambalo linajumuisha wananchi wa maeneo wa kata sita za Jimbo la Mtumba.

Akizungumza katika mkutano huo Ndg. Mavunde ametoa rai kwa wanakikundi hao kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuwachagua viongozi ambao watasimamia mustakabali wa maendeleo yao na ustawi wa jamii kwa miaka mitano ijayo.

Aidha Ndg. Mavunde alitumia fursa hiyo kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt. Samia S. Hassan na wagombea udiwani wote wa CCM.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa 𝙒𝘼𝙈𝙃𝘼𝙉𝙂𝘼 𝙁𝘼𝙈𝙄𝙇𝙔 Ndg. Motwa John Njilimuyi amesema wanakikundi kwa kutambua umuhimu wa uchaguzi mkuu watashiriki kikamilifu na kutimiza haki yao ya kikatiba ya kuwachagua viongozi kwa maendeleo yao.





No comments:

Post a Comment