
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kaspar Mmuya, tayari ameshapiga kura katika Kituo cha Zahanati kijiji cha Mtakuja, kilichopo Kata ya Nanganga, leo tarehe 29 Oktoba 2025.
Mmuya amepiga kura mapema asubuhi akiwa sambamba na wananchi wengine wa eneo hilo, akitimiza haki yake ya kikatiba kwa ajili ya kuwachagua Rais, Mbunge na Diwani.
Baada ya kupiga kura, Mmuya amewataka wananchi wote wa Ruangwa na Tanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kupiga kura kwa amani na utulivu.
Amesisitiza kuwa uchaguzi ni fursa muhimu ya kuamua mustakabali wa maendeleo ya nchi, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kikamilifu bila kujihusisha na vitendo vya vurugu au uchochezi.

No comments:
Post a Comment