MIAKA 26 BILA NYERERE; DKT. SAMIA ANASTAHILI PONGEZI KWA KULINDA AMANI NA UMOJA WA KITAIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 14, 2025

MIAKA 26 BILA NYERERE; DKT. SAMIA ANASTAHILI PONGEZI KWA KULINDA AMANI NA UMOJA WA KITAIFA


Tanzania tunapoadhimisha leo miaka 26 bila ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Amani na umoja ndizo tunu muhimu alizotuachia na zikisimamiwa kikamilifu na kwa nguvu kubwa na Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiamini kwamba umoja ndiyo nguvu ya mnyonge na amani ndilo chimbuko la maendeleo na ustawi wa Mtanzania na Taifa kwa ujumla.

Wakati chimbuko hilo la maendeleo ikitikiswa na watu wenye mtazamo tofauti kuhusu uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia, mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Tanzania mara zote tumemsikia akizungumza, kutoa miito ya ulinzi na kukumbusha kuhusu wajibu wa kila mmoja katika kulinda amani ya Tanzania, akisema siasa na uchaguzi havipaswi kuwa silaha ya kuangamiza amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

Kama ambavyo anasisitiza na kueleza dhamira yake ya kulinda tunu za Taifa na kutunza mema tuliyoachiwa na Baba wa Taifa, Dkt. Samia anasema fikra na falsafa za Mwalimu Nyerere zinapaswa kubakia kama dira ya Taifa, akikumbusha kuwa amani na umoja si zawadi bali ni matokeo ya misingi madhubuti ya Kitaifa.

Kwake Mwalimu Nyerere kama ilivyo kwa Dkt. Samia, aliamini kuwa Taifa haliwezi kusimama bila umoja na amani, alikataa siasa za chuki na ubaguzi wa kidini, Kikanda na Kijinsia na katika hotuba yake ya mwaka 1965 alinukuliwa akisema "sisi hatutaki siasa za kuwagawanya watu, tunataka uchaguzi uwe chombo cha mshikamano, siyo chanzo cha chuki."

Mwanasiasa mkongwe, Paul Kimiti amesema serikali ya awamu ya sita inastahili pongezi kwa namna ilivyoenzi maono na ndoto za Nyerere kwa kulifanya taifa kuwa tulivu, huku Watanzania wakiendelea kufanya kazi kwa ajili ya uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mwanahistoria nguli wa Tanzania, Mohamed Said amenukuliwa akisema kuwa Nyerere katika kusisitiza umuhimu wa amani na utulivu, aliwahusia Watanzania wasichoshwe na amani na kutamani vurugu. Amesema kutokana na maendeleo ya kisiasa katika mataifa mengine duniani kutawaliwa na vurugu za wenyewe kwa wenyewe, Nyerere aliamua kutoa tahadhari kuwa Watanzania muda wote wamekuwa katika kisiwa cha amani na utulivu, hivyo isitokee siku moja wakatamani kuipoteza.

“Mwalimu alifahamu kuwa kwa misingi waliyoijenga, kuipoteza amani ingekuwa vigumu sana kuipata tena. Ndio maana akahusia Watanzania wasichoke amani wakatamani vita,” ameongeza.

Amesema tangu limetolewa angalizo hilo, serikali zote zilizofuata ikiwemo ya Rais Samia zilijitahidi kulinda na kuimarisha amani na mshikamano akiamini kuwa maeneo na changamoto chache zilizobaki zitaendelea kushughulikiwa, kwani hakuna serikali yoyote duniani ambayo ilimaliza changamoto zake zote kwa wakati mmoja.

No comments:

Post a Comment