Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akipata maelezo mbalimbali wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.
Na Mwandishi Wetu – Arusha
Serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi na ufungaji wa mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, ikiwemo mtambo mdogo wa kuzalisha sukari uliopo Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, unaotarajiwa kuanza kazi Machi 2026. Mradi huo unalenga kuchochea uzalishaji na kuongeza kipato kwa wakulima wadogo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, ameyasema hayo Oktoba 20, 2025, alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo imetengeneza mtambo huo.
Bw.Mweli amesema kuwa ziara hiyo imelenga kujionea shughuli za uzalishaji wa mitambo na kujadili namna Wizara ya Kilimo inaweza kushirikiana na TEMDO katika kuwawezesha wanawake na vijana walioko chini ya Programu ya Kujenga Kesho Iliyobora.
Bw. Mweli amesema ujenzi na utengenezaji wa mitambo hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kukuza sekta ya kilimo kupitia matumizi ya teknolojia za ndani kwa gharama nafuu, ili kuchochea maendeleo na kuhakikisha miradi ya kimkakati inakamilika kwa wakati.
“Wizara yangu na taasisi zilizo chini yake tutaendelea kushirikiana na TEMDO katika kutumia mitambo ya kuongeza thamani ya mazao, ikiwemo mtambo huu wa kuzalisha sukari wenye uwezo wa kutengeneza tani 20 kwa siku. Hii ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuongeza ajira na kipato kupitia kilimo,” amesema Bw. Mweli.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Frederick Kahimba, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC), wamesema kuwa taasisi zao ziko tayari kushirikiana na Wizara ya Kilimo na taasisi zake kutengeneza mitambo itakayohitajika, kutoa ushauri wa kitaalamu, na kufanya matengenezo pale inapohitajika.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Bi. Irene Mlola, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Patrick M. Mongella, na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Bw. Primus Kimaryo, wameahidi kuendelea kushirikiana na TEMDO katika kuendeleza teknolojia za viwanda vinavyolenga kuwasaidia wakulima na kuongeza tija kwenye sekta ya kilimo.
Awali Mkurugenzi wa usanifu na utafiti wa TEMDO Mhandisi Nicas Bernard anasema anaona Faraja Taasisi yake ikifanikiwa kutatua changamoto mbalimbali kwa kutumia ubunifu na teknolojia kwa kutengeneza mitambo kulingana na mahitaji ya Wateja.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania, Bw. Primus Kimaryo,akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli (hayupo pichani) alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO, Profesa Frederick Kahimba,akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli (hayupo pichani) alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Bi. Irene Mlola,akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli (hayupo pichani) alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), Bw. Patrick M. Mongella,akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli (hayupo pichani) alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Mkurugenzi wa usanifu na utafiti wa TEMDO Mhandisi Nicas Bernard ,akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli (hayupo pichani) alipotembelea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akipata maelezo mbalimbali wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akipata maelezo mbalimbali wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akipata maelezo mbalimbali wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli,akipata maelezo mbalimbali wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea karakana ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) jijini Arusha, ambayo inatengeneza mitambo na mashine zitakazotumika kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

No comments:
Post a Comment