Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi Oktoba 25, 2025 amekutana na kuzungumza na Ujumbe wa Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika (AUEOM) ulioongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Botswana na Kiongozi wa Misheni hiyo, Mhe. Mokgweetsi Masisi, Ikulu ndogo ya Tunguu, Visiwani Zanzibar. Tanzania itafanya uchaguzi wake Mkuu Jumatano ya wiki ijayo Oktoba 29, 2025, Dkt. Samia akiwa miongoni mwa wanasiasa wanaowania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.






No comments:
Post a Comment