DKT. SAMIA AELEZA ULIVYOKUWA MCHAKATO WA KUMPATA WAZIRI MKUU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 14, 2025

DKT. SAMIA AELEZA ULIVYOKUWA MCHAKATO WA KUMPATA WAZIRI MKUU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Waziri Mkuu mpya wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kwa nafasi yake mpya ya utumishi, akisema jukumu lake la sasa ni kubwa na uteuzi wake umepitia ushindani mkubwa na katika vigezo kadhaa aliibuka mshindi kuliko wengine aliokuwa akishindana nao.


"Kubwa zaidi ni uwezo wa kuwatumikia wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi zako na maelekezo yote yamo kwenye Katiba na nimekukabidhi vitabu vinavyoelekeza majukumu yako." Amenukuliwa akisema Rais Samia.


Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Novemba 14, 2025 Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma, mara baada ya kumuapisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa 14 wa Tanzania akichukua nafasi ya Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyeitumikia nafasi hiyo kwa takribani miaka kumi ikiwemo Mitano chini ya serikali ya Rais Samia.


Dkt. Samia amemshukuru pia Mhe. Majaliwa kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta ya elimu, afya na mambo mengineyo, akisema amekuwa msaidizi mzuri katika kipindi chote alichofanya kazi kwenye serikali ya awamu ya sita.

No comments:

Post a Comment