
Askari wa Kikosi cha kutuliza Ghasia wakiwa katika Gwaride maalumu ambalo litakaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuhutubia na kufungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Ijumaa Novemba 14, 2025.
Dkt. Samia anatarajiwa alasiri hii kuzindua Bunge hilo mara baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akitarajiwa kutumia hotuba yake kueleza muelekeo, vipaumbele na mtindo wa serikali yake katika kipindi cha miaka mitano ijayo saa chache mara baada ya kumuapisha Waziri Mkuu wake Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Ikulu ya Chamwino.


No comments:
Post a Comment