MHANDISI SEFF AELEZA JITIHADA ZA TARURA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 16, 2025

MHANDISI SEFF AELEZA JITIHADA ZA TARURA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI



Na Mwandishi Wetu, Belem, Brazil


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada kubwa ambayo imeweza kukamilisha miundombinu iliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mengi.

Mhandisi Seff ameeleza hayo wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa 30 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP 30) unaoendelea katika Jiji la Belem nchini Brazil.

Aidha, katika wasilisho lake Mtendaji Mkuu huyo aliweza kuonesha Makala fupi ya namna Wakala huo ulivyofanikiwa kurudisha mawasiliano ya miundombinu ya barabara iliyoharibika kwa kujenga miundombinu himilivu ‘resilient’ kwa athari za mabadiliko ya tabianchi na zenye uwezo wa kupitika mwaka mzima.

Amesema kupitia programu ya uondoaji vikwazo katika barabara (bottleneck), wameweza kujenga madaraja na barabara na hivyo kufungua mawasiliano katika vijiji na hivyo kuweza kuwasaidia wananchi kusafirisha mazao yao pia kuwarahisishia kupata huduma za kijamii zikiwemo huduma za afya.

Akichangia kwenye mradi wa Scale unaosimamiwa na TAMISEMI, amesema TARURA ni mdau mkubwa kwenye mradi huo.




No comments:

Post a Comment