TETESI ZA SOKA ULAYA : BARCELONA YAJIPANGA KUMPA RASHFORD MKATABA WA KUDUMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, November 6, 2025

TETESI ZA SOKA ULAYA : BARCELONA YAJIPANGA KUMPA RASHFORD MKATABA WA KUDUMU


Real Madrid imejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili Mchezaji wa Crystal Palace Marc Guehi, 25, ambaye kandarasi yake inamalizika msimu huu wa joto kwa sababu ya mshahara mkubwa na mahitaji mengine, huku Liverpool na Bayern Munich wakipigiwa upatu kumnunua mlinzi huyo wa Uingereza. (AS - kwa Kihispania)

Vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vina nia ya kumsajili beki wa Feyenoord Mholanzi Givairo Read mwenye umri wa miaka 19 lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich. (Teamtalk)

Tottenham na Liverpool zinamnyatia beki wa Ugiriki anayekipiga Wolfsburg Ujerumani Konstantinos Koulieraki, 21. (TBR Football)

Meneja wa Barcelona Hansi Flick hana nia ya kuondoka katika klabu hiyo msimu ujao wa joto licha ya ripoti kutoka Uhispania kwamba "amechoshwa" na klabu hiyo na anapanga kujiuzulu. (Sky Germany - kwa Kijerumani)

Leeds inakabiliwa na kibarua cha kuhifadhi huduma za mlinda lango Mwingereza Alex Baird, 18, zaidi ya Januari huku vilabu kadhaa vikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Caught Offside)


Kalabu ya Barcelona inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 28, kwa mkataba wa kudumu, lakini hawawezi kumudu bei pauni milioni 25.5 ikatika mkataba wake wa mkopo. (Fichajes - kwa Kihispania)

Juventus inapanga kuanzisha mazungumzo ya mkataba na vilabu vya Liverpool, Chelsea na Arsenal vinavyomuwania Kenan Yildiz, 20, lakini klabu hiyo inatarajia mshambuliaji huyo wa Uturuki atasalia Turin. (Teamtalk)


Roma inajiandaa kuwasilisha ofa ya mkopo ikiwa na chaguo la kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, mwezi Januari. (Fichajes - kwa Kihispania)

No comments:

Post a Comment