𝗠𝗔𝗥𝗘𝗞𝗔𝗡𝗜 𝗜𝗠𝗥𝗨𝗗𝗜𝗦𝗛𝗘 𝗠𝗔𝗡𝗚E 𝗞𝗜𝗠𝗔𝗠𝗕𝗜, 𝗔𝗡𝗔 𝗞𝗘𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗕𝗨 - 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗘 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 17, 2025

𝗠𝗔𝗥𝗘𝗞𝗔𝗡𝗜 𝗜𝗠𝗥𝗨𝗗𝗜𝗦𝗛𝗘 𝗠𝗔𝗡𝗚E 𝗞𝗜𝗠𝗔𝗠𝗕𝗜, 𝗔𝗡𝗔 𝗞𝗘𝗦𝗜 𝗭𝗔 𝗞𝗨𝗝𝗜𝗕𝗨 - 𝗠𝗖𝗛𝗔𝗡𝗚𝗘



"Mbegu za vurugu za tarehe 29 Oktoba na hizi wanazoendelea kuhamasishana zinatokana na baadhi ya wanaharakati waishio nje ya Tanzania ambao wapo Kenya na Marekani"

"..wanaochochea vurugu, mauaji na kutokuheshimika kwa mamlaka za nchi wapo huko kwenye hayo mataifa yao, sisi kama MECIRA hatutakaa kimya na tutaendelea kulisema hili kwakuwa kinachofanyika ni kuvuruga amani ya nchi yetu."

"hao wanaochochea wanafahamika mahali wanapoishi katika hizo nchi, tumeziomba balozi ziturudishie hao watu, hili jambo si serikali peke yake bali watanzania kwa pamoja lazima tuungane kuipigania Tanzania, hawa watu lazima warejeshwe nchini kujibu kesi hizi za kusababisha vurugu"

"hii ni kama rushwa, aliyetoa na aliyepokea, wao ni sehemu ya matokeo ya vifo vilivyotokea kutokana na vurugu hizo walizozipanga, hakuna haki bila wajibu."

"tunafahamu Maria Sarungi amekimbia Nairobi huko Kenya na kukimbilia Skandinavia, tutamfata, tutaenda kuwashtaki mpaka mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC), lazima hawa watu wanaochochea lazima wakamatwe"

Bw. 𝗛𝗮𝗯𝗶𝗯𝘂 𝗠𝗰𝗵𝗮𝗻𝗴𝗲
Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari watetezi wa Rasilimali za Taifa

Mkutano na Wanahabari
🗓️17 Disemba 2025

No comments:

Post a Comment