
Lilongwe, Malawi
Hospitali ya Benjamin Mkapa(BMH) imefungua ukurasa mpya wa kupanua mashirikiano na Serikali ya Malawi kupitia Wizara ya Afya katika maeneo ya kuboresha Matibabu ya Kibobezi, Mafunzo ya Watalamu na Tafiti ili kunufaisha Wananchi wa pande zote kufuatia mazungumzo ya awali kati ya Watalaamu wa BMH wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Prof Abel Makubi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Malawi , Dr Dan Namarika chini ya Uratibu wa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe Agnes Kayora.
Watalaamu kutoka BMH walitembelea Hospitali nne za hospitali ya Kamuzu (Lilongwe), Queen Elizabeth (Blantiyre), Zomba na Mzuzu nchini Malawi baaadae kukutana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Dkt. Dan Namarika.
Katika mazungumzo ya pande zote, BMH itasaidia katika utalii wa matibabu, kujengea uwezo watalamu kupitia mafunzo, kambi za matibabu na kushirikiana katika kubadilishana uzoefu na Tafiti. Uongozi wa wizara ya Afya pia umevutiwa sana na uwekezaji wa serikali ya Tanzania katika huduma za kibobezi hasa upandikizaji Figo, uloto, upasuaji wa Moyo, ubongo , mfumo wa mkojo na ubadilishaji wa goti na nyonga , na kuahidi kuitembelea BMH mwakani kupata uzoefu katika maeneo ya haya, uendeshaji wa Mifumo ya Uongozi ya Hospitali na Upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.





No comments:
Post a Comment