IAA KUWEKEZA BILIONI NNE KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UFUNDISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 20, 2025

IAA KUWEKEZA BILIONI NNE KUBORESHA MIUNDOMBINU YA UFUNDISHAJI

  


Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA), Prof. Eliamani Sedoyeka amesema zaidi ya shilingi bilioni nne zimetengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia. 

Prof. Sedoyeka ameyasema hayo Disemba 09, 2025 katika mahafali ya 27 ya IAA yaliyofanyika katika Kampasi ya Arusha ambapo jumla ya wahitimu 4821 wamehitimu ngazi ya astashahada, stashaahda na shahada katika fani mbalimbali. 

Amesema katika kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia  chuo kimeanza utekelezaji wa mpango wa madarasa janja (Smart Class) kwa lengo la kuwa na kampasi janja (Smart Campus) na kutumia TEHAMA kikamilifu katika ufundishaji, kutumia mifumo ya kisasa ya kidijitali na kujifunzia kwa njia ya mtandao. 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi. Mshamu Ali Munde amesema soko la ajira linabadilika kwa kasi kutokana na teknolojia, usimamizi wa kisasa na mifumo ya kidigitali, hivyo ameipongeza IAA kwa kuboresha miundombinu, kuandaa mitaala inayoendana na soko la ajira na kuandaa  wataalam mahiri wanaokidhi viwango vya kimataifa.

Aidha Mhe. Munde amewaambia wahitimu kuwa , “Mmeandaliwa vizuri nendeni mkalete mabadiliko katika sekta mnazokwenda kutumikia.Katumieni elimu mliyopata IAA kama nyenzo ya kujijenga kimaisha na kiteknolojia, kuchochea maendeleo ya familia zenu, na kuwa chachu ya maendeleo ya taifa letu”.

 Naye Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, Dkt. Mwamini Tulli, amesema IAA inaendelea kuboresha na kupanua miundombinu ya kufundishia na katika kampasi zake za Arusha, Babati, Dar es Salaam, Dodoma na Songea na kinaendelea kujipanga kuwekeza nguvu na rasilimali katika ujenzi wa kampasi mpya ya Bukombe iliyoanza rasmi mwaka huu wa masomo.













No comments:

Post a Comment